Yesu Ndiye Mfalme: Mathayo 1-7 (Paperback)

Yesu Ndiye Mfalme: Mathayo 1-7 By Rev Dr Gerson Mgaya Cover Image

Yesu Ndiye Mfalme: Mathayo 1-7 (Paperback)

$10.00


Not On Our Shelves—Ships in 1-5 Days
(This book cannot be returned.)
Mathayo aliiandika Injili hii akiwa na lengo la kuwafundisha watu juu ya jambo moja: Yesu ndiye Mfalme. Wayahudi walikuwa wameahidiwa angewajia Masihi na hivyo walikuwa wanaisubiri ahadi hiyo. Mathayo anawaandikia akiwaambia kuwa Masihi waliyekuwa wameahidiwa ameshakuja na masihi huyo ni Yesu. Habari zake zimeenea kwa sasa karibu pande nyingi za dunia watu wamesikia habari za Yesu na makanisa mengi yameanzishwa kama itikio la habari hizo. Lakini kwa siku za sasa limejitokeza tatizo moja kubwa ambalo tusipolishughulikia, hali itaendelea kuwa mbaya siku kwa siku. Ufalme wa Yesu katika maisha ya watu haudhihiriki kama inavyotakiwa. Maisha ya waliompokea Yesu kama mfalme wao hayaoneshi kuwa yanatawaliwa naye. Hii inaweza kuwa ni kwa sababu ufalme wake katika maisha ya watu haujafafanuliwa. Ni vipi wasiyemwona kwa macho anaweza kuwa mtawala wao? Kwa hiyo, moja ya lengo la kitabu hiki ni kufafanua ufalme wa Yesu ambao Mathayo anauandika katika Injili ya Mathayo ni ufalme wa aina gani, na waupokeao ufalme huo maisha yao huwaje. Ulimwengu tulio nao umewadanganya watu kiasi cha kuwafanya wapoteze maana ya ufuasi wao kwa Yesu. Ninaamini kwamba umalizapo kukisoma kitabu hiki hutajutia kwamba ulitumia muda wako kwa kukisoma, badala yake utasikitika kwamba kitabu hiki kimechelewa kukujia. Mungu akujalie kuzisoma habari za Mfalme Yesu ili ikiwa bado hajapata nafasi stahiki katika maisha yako, basi aipate mara moja. Roho wa Bwana na awe juu yako katika usomaji wako, Ameni.
Product Details ISBN: 9781976445408
ISBN-10: 197644540X
Publisher: Createspace Independent Publishing Platform
Publication Date: September 27th, 2017
Pages: 202
Language: Swahili